Mafunzo

Mafunzo

Vipaumbele katika Mafunzo ya Kituo cha Urithi wa Ukombozi wa Afrika

  1. Kujenga Uwezo wa Wataalamu: Kuendesha mafunzo endelevu kwa wataalamu wa urithi, makavazi na nyaraka kuhusu mbinu bora za uhifadhi na usimamizi wa urithi.

  2. Elimu ya Historia ya Ukombozi wa Afrika: Kutoa mafunzo yanayoongeza uelewa wa historia, falsafa na mchango wa harakati za ukombozi wa Afrika.

  3. Uhifadhi na Uwekaji wa Kumbukumbu Kidijitali: Kukuza ujuzi wa matumizi ya teknolojia katika uhifadhi, uorodheshaji na usimamizi wa kumbukumbu za urithi.

  4. Utafiti na Ubunifu: Kuimarisha uwezo wa kufanya tafiti na kuandaa machapisho yanayohusu urithi wa ukombozi wa Afrika.

  5. Elimu kwa Umma na Vijana: Kuandaa programu za mafunzo na uelimishaji zinazokuza uzalendo, utambulisho wa Kiafrika na utunzaji wa urithi.

  6. Ushirikiano na Kubadilishana Uzoefu: Kukuza mafunzo ya pamoja na taasisi za urithi, makavazi, vyuo vikuu na wadau wa ndani na kimataifa ili kubadilishana maarifa na uzoefu.

lbl_need_any_help