Kuhifadhi na Kutangaza Kituo cha Urithi wa Ukombozi wa Afrika
Vipaumbele katika Kulinda, Kuhifadhi na Kutangaza Kituo cha Urithi wa Ukombozi wa Afrika
- Uhifadhi Endelevu wa Urithi; Kuhifadhi nyaraka, vielelezo, kumbukumbu na maeneo ya kihistoria kwa kuzingatia viwango vya kitaalamu vya uhifadhi wa urithi.
- Uwekaji wa Kumbukumbu Kidijitali; Kufanya uhakiki, uwekaji wa kumbukumbu na ujanibishaji wa taarifa kwa matumizi ya utafiti na kizazi kijacho.
- Utafiti na Uzalishaji wa Maarifa; Kuendeleza tafiti kuhusu historia ya ukombozi wa Afrika na kuchapisha matokeo yake ili kuongeza uelewa wa jamii.
- Elimu na Uhamasishaji wa Umma; Kukuza uelewa wa wananchi, hususan vijana, kupitia maonesho, programu za elimu na shughuli za urithi.
- Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa; Kuimarisha ushirikiano na nchi za Afrika, taasisi za urithi na wadau wa maendeleo katika kuhifadhi na kutangaza urithi wa ukombozi.
- Utangazaji na Utalii wa Urithi; Kutumia majukwaa ya kidijitali na vyombo vya habari kutangaza Kituo kama kitovu cha historia, elimu na utalii wa urithi wa Afrika.