Changia
Kituo cha Urithi wa Ukombozi kinawakaribisha kwa heshima taasisi, mashirika, jumuiya, vikundi na watu binafsi kuchangia taarifa, nyaraka, kumbukumbu na mikusanyo yenye thamani ya kihistoria kuhusu harakati za urithi wa ukombozi wa Bara la Afrika. Mchango wako wa thamani utasaidia kuhifadhi, kulinda na kuendeleza urithi wa ukombozi, pamoja na kuimarisha utafiti, elimu na uenezaji wa historia na maarifa kwa manufaa ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo, Kituo kinathamini na kutambua mchango wa kila mdau katika juhudi za kuhifadhi urithi wetu wa pamoja, ili kuuenzi na kuurithisha kwa vizazi vya sasa na vijavyo kwa maendeleo endelevu ya taifa.