Huduma Tunazotoa

Huduma Tunazotoa

  1. Kutoa elimu kwa umma yenye kuchochea uzalendo, umoja na mshikamano kupitia majukwaa mbalimbali yakiwemo matamasha, maonesho, midahalo, makongamano, vyombo vya habari na katika mitandao ya kijamiii;
  2. Kunadi na kutoa taarifa za maeneo ya utalii wa kiukombozi yaliyopo nchini;
  3. Kuonesha kumbukumbu zinazoshikika na zisizoshikika za historia ya ukombozi wa Afrika kupitia Makumbusho yenye vifaa na vielelezo mbalimbali vilivyotumika wakati wa harakati za ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika;
  4. Kutoa elimu kupitia Maktaba yenye nyaraka mbalimbali za historia ya ukombozi wa bara la Afrika zikiwemo Vitabu, Majalida, Makala, Magazeti, Hotuba za sauti na Makala jongefu pamoja na nyimbo za kiukombozi zilizokuwa zikihamasisha harakati hizo; na
  5. Huduma zingine zinazotolewa na Kituo ni pamoja na tafiti kwa wataalamu mbalimbali, kukodisha ukumbi wa mikutano, upigaji wa picha za kumbukumbu na huduma ya kutembelea maonesho yenye vielelezo vya picha mbalimbali za kihistoria.
lbl_need_any_help