Uratibu
a) Kuratibu, kusimamia na kushiriki katika maonesho, matamasha, warsha na vikao kazi ili kutoa elimu kwa umma kuhusu urithi wa ukombozi wa Afrika.
b) Kuratibu na kusimamia uanzishwaji wa Kituo Kikuu cha Urithi wa Ukombozi wa Afrika.
c) Kuhamasisha nchi wanachama kuanzisha matawi ya programu ya urithi wa ukombozi wa Afrika na kufuatilia utekelezaji wake.
d) Kukijengea uwezo Kituo, wataalamu na wadau wa urithi wa ukombozi ili kusimamia, kuhifadhi na kuendeleza urithi wa ukombozi wa Afrika.
e) Kutekeleza maelekezo ya Sera ya Taifa ya Utamaduni na maazimio ya mikataba ya kikanda na kimataifa kuhusu uhifadhi na uendelezaji wa urithi wa ukombozi wa Afrika.