Tafiti
Utafiti – Kituo cha Urithi wa Ukombozi wa Afrika (ALHC)
Utafiti katika Kituo cha Urithi wa Ukombozi wa Afrika (ALHC) kinalenga kuzalisha, kuhifadhi na kuendeleza maarifa kuhusu historia ya ukombozi wa Afrika, urithi wake na maendeleo ya kijamii na kisiasa. Kupitia tafiti za kitaalamu, ukusanyaji wa nyaraka na ushirikiano na watafiti pamoja na taasisi mbalimbali, ALHC huchangia katika kuhifadhi kumbukumbu za kihistoria, kuimarisha elimu, na kusaidia maamuzi yanayotegemea ushahidi kwa ajili ya maendeleo endelevu ya bara la Afrika.