Kituo na Taasisi ya SISI ni Hazina Creative zaweka...

Kituo na Taasisi ya SISI ni Hazina Creative zaweka mikakati ya pamoja ya kutangaza urithi wa ukombozi nchini.

5 Agosti, 2026
Kituo na Taasisi ya SISI ni Hazina Creative zaweka mikakati ya pamoja ya kutangaza urithi wa ukombozi nchini.

Kituo cha Urithi wa Ukombozi wa Afrika na Taasisi ya Sisi ni Hazina Creative zimekubaliana kwa pamoja kushirikiana katika kutangaza na kutoa elimu ya historia ya ukombozi kwa umma kupitia majukwaa ya mitandao ya kijamii kwa lengo la kuendelea kurithisha urithi wa ukombozi kwa kizazi cha sasa na kijacho.

Makubaliano hayo yamefikiwa leo tarehe 04 Agosti, 2026 katika kikao cha pamoja baina ya Kituo na uongozi wa taasisi ya Sisi ni Hazina Creative kilichofanyika katika ofisi za Kituo Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujadili namna ya kushirikiana katika kutangaza historia kwa jamii.

Aidha, Kituo na taasisi hiyo zimekubaliana kuifikia hadhira kubwa hasa vijana kurithisha na kuhamasisha kutembelea vivutio vya utalii wa kihistoria vilivyopo nchini ili kuongeza uelewa mpana kuhusu historia ya harakati za ukombozi wa Afrika.

lbl_need_any_help