Wizara Yajipanga Kikamilifu Kuelekea Tamasha la Nn...

Wizara Yajipanga Kikamilifu Kuelekea Tamasha la Nne la Kitaifa la Utamaduni 2026.

24 Julai, 2026
Wizara Yajipanga Kikamilifu Kuelekea Tamasha la Nne la Kitaifa la Utamaduni 2026.

Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imefanya kikao cha maandalizi kwa lengo la kupitia na kuratibu hatua mbalimbali utekelezaji kuelekea Tamasha la Nne la Kitaifa la Utamaduni, litakalofanyika kuanzia tarehe 25 hadi 29 Agosti 2026.

Kikao hicho kimefanyika leo, Julai 23, 2026, katika Kituo cha Urithi wa Ukombozi wa Afrika, jijini Dar es Salaam, kikiongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Methusela Ntonda.

lbl_need_any_help