Habari
KAMATI YA BUNGE YAPONGEZA JUHUDI ZA UHIFADHI URITHI WA UKOMBOZI WA BARA LA AFRIKA
KAMATI YA BUNGE YAPONGEZA JUHUDI ZA UHIFADHI URITHI WA UKOMBOZI WA BARA LA AFRIKA
Kamati ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo imekipongeza Kituo cha Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika kilichopo jijini Dar es Salaam kwa kukarabati jengo la Historia ya Ukombozi wa Bara hilo pamoja na kuhifadhi vyema kumbukumbu za Wapigania Uhuru.
Hayo yamejiri leo Machi 18, 2023 wakati wa ziara ya Kamati hiyo katika Kituo hicho kuona utekelezaji wa Bajeti ya mwaka wa fedha 2021/22 iliyotengwa kwa ajili ya utekelezaji wa Majukumu ya Kituo hicho
Makamu mwenyikiti wa Kamati hiyo Mhe. Husna Sekiboko,(Mb) amesema kwamba, Historia hiyo lazima iingizwe katika mitaala ya Shule na Vyuo Vikuu ili Wanafunzi ambao ndio kizazi cha kesho wafahamu na kutambua mchango wa Tanzania katika kusaidia nchi za Afrika kujikomboa.
"Tanzania imesaidia nchi nyingi kujikomboa, ni vyema nchi hizo zikatambua mchango huu ambao Taifa letu limeufanya ili kuimarisha uhusiano wetu" amesema Mhe.Sekiboko.
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo amesema mpaka sasa Kituo hicho kimetambua maeneo 260 ambayo yalitumika katika harakati hizo, huku akisisitiza kuwa Wizara itaendelea kukusanya taarifa mbalimbali kuhusu historia hiyo katika maeneo mbalimbali na kuyatangaza katika Gazeti la