Habari
ZIARA YA WAZIRI WA UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akipokea maelezo kutoka kwa Mratibu wa Kituo Cha Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika Bw. Boniface Kadili alipotembelea Kituo hicho Februari 23, 2023 jijini Dar es Salaam. Katika ziara hiyo ya kwanza tangu ateuliwe kuongoza Wizara hiyo, Waziri Balozi Dkt. Pindi Chana ameambatana na Naibu Waziri Mhe. Pauline Gekul na Mkurugenzi wa Idara Maendeleo ya Utamaduni Dkt. Emmanuel Temu.