Kituo Na UDOM kuendelea kuimarisha ushirikiano kat...

Kituo Na UDOM kuendelea kuimarisha ushirikiano katika uendelezaji wa Historia Ya Ukombozi wa Afrika.

22 Septemba, 2026
Kituo Na UDOM kuendelea kuimarisha ushirikiano katika uendelezaji wa Historia Ya Ukombozi wa Afrika.

Kituo cha Urithi wa Ukombozi wa Afrika kimefanya kikao na Prof. Zuhura Badru, Rasi wa Ndaki ya Insia na Sayansi za Jamii kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kwa lengo la kujadili na kuimarisha ushirikiano kati ya pande mbili katika maeneo ya utamaduni, utafiti na urithi wa historia ya ukombozi wa Afrika.

Kikao hicho kilichojadili fursa mbalimbali za ushirikiano kimefanyika Septemba 17, 2026 katika ofisi za Kituo cha Urithi wa Ukombozi wa Afrika Jijini Dar es Salaam na kuongozwa na Mratibu wa Kituo hicho, Bw. Christopher Mhongole.



Pamoja na kikao hicho, Prof. Badru alitembelea na kujionea makavazi ya Kituo yaliyosheheni urithi wa historia ya harakati za ukombozi wa Afrika. Aidha, Prof. Badru alipata wasaa wa kusalimiana na wanafunzi wa UDOM wanaofanya mafunzo kwa vitendo Kituoni hapo ikiwa ni sehemu ya kutambua ushirikiano uliopo baina ya pande zote mbili.

Ushirikiano wa Kituo na UDOM unalenga kuendeleza tafiti, elimu, kutangaza na uhifadhi wa urithi wa ukombozi wa Afrika kwa manufaa ya kizazi cha sasa na vijavyo.

lbl_need_any_help