KAMBI YA KONGWA | DODOMA

KAMBI YA KONGWA | DODOMA

Tanzania
KAMBI YA KONGWA | DODOMA
Kongwa ni moja ya maeneo muhimu ya Kituo cha Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika, yanayohifadhi historia ya mchango wa Tanzania katika harakati za ukombozi wa Bara la Afrika. Kuanzia mwaka 1964, eneo hili lilitengwa na Serikali ya Tanzania kwa ajili ya makambi ya mafunzo na makazi ya wapigania uhuru waliotambuliwa na Kamati ya Ukombozi ya Organization of African Unity. Makundi ya ukombozi yaliyoweka kambi Kongwa ni pamoja na; FRELIMO, ANC, PAC, SWAPO NA ZANU PF • South West Africa People's Organization – Namibia • Frente de Libertação de Moçambique – Msumbiji • African National Congress – Afrika Kusini • Movimento Popular de Libertação de Angola – Angola • Zimbabwe African People's Union – Zimbabwe Maeneo ya kihistoria yanayopatikana Kongwa ni pamoja na: • Mabweni yaliyotumiwa na wapigania uhuru. • Viwanja vya mafunzo ya kijeshi na kisiasa. • Mahandaki (trenches) na maeneo ya mazoezi. • Makaburi ya baadhi ya mashujaa wa ukombozi. • Majengo na miundombinu iliyohifadhiwa kama sehemu ya urithi wa ukombozi wa Bara la Afrika.
lbl_need_any_help