Kampasi Ya Solomon Mahlangu (SMC)
Kampasi ya Solomon Mahlangu ambayo ni Kampasi ya pili ya Chuo Kikuu cha Sokoine ipo Manispaa ya Morogoro. Ilianzishwa kuwa shule ya wapigania uhuru wa chama cha African National Congress cha Afrika Kusini mwaka 1978. .
Kampasi ipo: .
Kijiji cha Mazimbu.
Kata ya Mazimbu.
Tarafa ya Kihonda.
Manispaa ya Morogoro Mjini.
Hali ilivyokuwa.
Jina la chuo wakati huo lilikuwa ni Shule ya ANC Mazimbu. Kutokana na mchango mkubwa wa SOLOMON MAHLANGU kwenye harakati za ukombozi, chama cha ANC kiliamua kubadili jina la Shule hiyo kuwa “SOLOMON MAHLANGU FREEDOM COLLEGE” (SOMAFCO). Jina hilo liliendelea hadi mwaka 1992 wakati wapigania uhuru wa ANC walipoanza kurudi kwao. .
Kituo kikiwa chini ya serikali ya Tanzania kilibadili jina na kuwa kituo cha Mazimbu cha Teknolojia na Elimu ya Juu. .
Tarehe 31 Mar 1999 baraza la Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo katika kikao chake cha 60 liliamua kukiita kituo cha Mazimbu, KAMPASI YA SOLOMON MAHLANGU (Solomon Mahlangu Campus) kwa kutambua mchango wa kituo hiki kwenye harakati za ukombozi Afrika ya Kusini.