Hali ilivyokuwa
Ofisi Maalum ya JWTZ iliyosimamia mafunzo ya kijeshi na kuratibu mambo ya utawala kwa wapigania uhuru ilikuwepo nyuma ya ofisi ya Mkuu wa Wilaya Iringa mjini.
Ipo katika:-
Mtaa wa Bomani
Kata ya Gangilonga
Tarafa ya Iringa Mjini
Manispaa ya Iringa Mjini
Hali ilivyo sasa
Baada ya shughuli za Kikosi Maalum kukoma ofisi ilikabidhiwa kwa Mshauri wa Mgambo na Ustawi wa Jamii.
Kuna maeneo matatu katika Mkoa wa Pwani yaliyohusika na shughuli za wapigania uhuru. Maeneo hayo ni Kidogozero, Kaole na Pongwe Msungura.