The Ladha Meghji Indian Public Library” ni jengo lililojengwa mwaka 1933 mjini Mwanza wakati wa ukoloni wa Mwingereza kuwa maktaba ya watu wenye asili ya Kiasia.
Wakati wa harakati za ukombozi wa nchi za Afrika, viongozi wa Kiafrika akiwemo hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na hayati Tom Mboya wa Kenya walipendekeza kufanyika mkutano wa pamoja wa shrikisho lililoundwa kuhamasisha nchi za Afrika Mashariki, Kati na Kusini kudai uhuru lililoitwa Pan African Freedom Movement for East and Central Africa (PAFMECA) Mkutano ulifanyika katika maktaba hii mwezi Mei 1958.
Mahali jengo lilipo
Karibu na Mwanza Hotel
Mtaa wa Posta
Kata ya Nyamagana
Tarafa ya Nyamagana
Wilaya ya Nyamagana